4G KUTOKA KWA CHELSEA YAMFUKUZISHA KAZI TONY PULLIS WEST BROM

West Brom have sacked Tony Pulis following their 4-0 thrashing by Chelsea at the weekend 
Siku mbili baada ya kupokea kichapo cha bao 4-0 toka kwa Chelsea nyumbani, klabu ya West Browmwich Albion imemtimua kocha wake mkuu Tony Pullis baada ya kushindwa kufikia matarajio ya klabu.


Mlimiliki wa klabu hiyo Mchina Guochuan Lai alikua uwanjani Hawthorns akishuhudia timu yake ikizidiwa kila idara na mabingwa watetezi Chelsea siku ya Jumamosi na bila kupoteza muda uamuzi wa kumtimua kocha huo ulifikiwa na leo kutoka taarifa ya kufukuzwa kazi.

Mashabiki walionekana kutoridhishwa na matokeo ya Jumamosi mpaka kufikia wengine kuimba na kubeba mabango ya kushinikiza atimuliwe kazi kocha huyo wa Zamani wa Stoke City.

Pullis amekua na matokeo mabaya katika ligi kuu akishinda mara mbili tu katika mechi 21 za ligi kuu ya England ikiiweka West Brom katika nafasi ya 17 ikiwa na pointi 10 tu mpaka sasa.



No comments

Powered by Blogger.