SIMBA: NJOONI MUWEKEZE NYARAKA ZIKO TAYARI

Kamati inayoshughulikia masula ya zabuni ya klabu ya Simba imetangaza kukamilika kwa nyaraka za mwaliko wa awali (Expression of Interest) na kuwataka wanachama wenye sifa kujitokeza.

Mkutano mkuu maalum wa klabu hiyo uliofanyika Agosti 20 mwaka huu ulipitisha azimio la kuanzisha na kutekeleza mchakato wa uwekezaji uliopitiswa.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti huyo, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema nyaraka hizo zimekamilika na amewataka wanachama wenye nia ya dhati ya kutaka kuwekeza kujitokeza kwa wingi.

Zoezi la kuchukua nyaraka hizo litakamilika Oktoba 18 ambalo litatangazwa kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa kwa wazabuni watarajiwa kujiandaa, kukamilisha nyaraka muhimu na kufanya mashauriano kabla ya kuwasilisha. Zoezi hilo litachukua siku 10.

Jaji Mihayo alisema "Nyaraka za mwaliko wa zabuni zimekamilika. Niwakaribishe wanachama wa klabu ya Simba wenye sifa kujitokeza kabla ya kufungwa kwa zoezi hili".


Mwenyekiti huyo pia alisema watakuwa wanatoa taarifa kupitia vyombo vya habari katika kila hatua ya mchakato huo mpaka apatikane mshindi.

No comments

Powered by Blogger.