IKIWA NA WATU LAKI 3 TU ICELAND INAKARIBIA KUTINGA KATIKA KOMBE LA DUNIA

Iceland competed in their first major tournament at Euro 2016
Timu ya Taifa ya Iceland jana ilijiweka katika nafasi nzuri ya kushiriki kwa mara ya kwanza katika fainali za kombe la dunia ikiifunga Uturuki nyumbani kwao kwa bao 3-0.

Iceland ambayo kwa mara ya kwanza ilishiriki mashindano makubwa mwaka jana wakati waliposhiriki fainali za Euro 2016 nchini Ufaransa

Nchi hiyo ambayo ina watu laki 3 tu inaweza kupata nafasi ya kushiriki fainali zijazo za kombe la dunia kama wataifunga Kosovo jumatatu wakati Iceland itakapokua katika uwanja wake wa nyumbani

Timu hiyo inaongoza katika kundi I ikiwa na pointi 19 ikifuatiwa na Croatia wenye pointi 17.

No comments

Powered by Blogger.