MAN UNITED YAPATA MTEREMKO KOMBE LA LIGI, ARSENAL YAKABIDHIWA NA WEST HAM. RATIBA KAMILI HII HAPA.
Droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Ligi nchini England maarufu kama Carabao Cup imepangwa jioni hii huku timu 8 zilizoingia hatua ya robo fainali zikipata ratiba zao.
Mabingwa watetezi Manchester United wamepangwa kucheza mechi Yao ya robo fainali ugenini dhidi ya Bristol City timu kutoka Ligi daraja la kwanza nchini England Ikiwa ni timu pekee ya kutoka Ligi daraja la chini huku timu zingine zote zikiwa ni za ligi kuu.
Arsenal baada ya kuitupa nje Everton itakua na kibarua kigumu kuikabili West Ham United ambayo imetinga hatua hii baada ya kuiondosha Tottenham Kwa bao 3-2 mechi ikitarajiwa kupigwa katika dimba la Emirates.
Chelsea wenyewe wamepangwa kucheza dhidi ya AFC BOURNEMOUTH Katika mchezo mwingine wa hatua hii ambapo watakua nyumbani wakati Manchester City watasafiri mpaka Leicester kuwakabili Leicester City katika dimba la King Power.
Ratiba ya Robo fainali ya michuano hiyo inaonyesha mechi hizo zitachezwa Disemba 19 na 20 mwaka huu huku Fainali imepangwa kuwa Februari mwakani.

No comments