KUZIONA SIMBA,YANGA BUKU KUMI

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika wikiendi ujao katika uwanja wa Uhuru.

Viingilio hivyo vitakuwa sh 20,000 kwa jukwaa kuu na sh 10,000 kwa mzunguko katika uwanja huo wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 23,000.

Ofisa habari wa Shirikisho hilo Alfred Lucas alitangaza viingilio hivyo alisema"kiingilio cha chini kwenye mchezo namba 58 kati ya Yanga dhidi ya Simba kitakuwa sh 10,000 na cha juu kitakuwa sh 10,000.
Moja ya kivutio kikubwa kwenye mchezo huo kitakuwa ni washambuliaji Emmanuel Okwi wa Simba ambaye ndiye kinara wa ufungaji akiwa na mabao manane na Ibrahim Ajib wa Yanga aliyefunga mabao matano.

Simba ina rekodi nzuri kuelekea mchezo huo baada ya kushinda mechi tatu mfululizo zilizopita dhidi ya watani wao.

No comments

Powered by Blogger.