ARSENAL YAPATA USHINDI MUHIMU NYUMBANI
Mechi ya ligi kuu nchini England baina ya wenyeji Arsenal dhidi ya wageni katika ligi hiyo Brighton & Hove Albion kwa wenyeji Arsenal kushinda bao 2-0.
Beki Nacho Monreal alitangulia kuipatia Arsenal bao la kwanza dakika ya 16 tu ya mchezo bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kiliwanufaisha zaidi wenyeji ambao walijipatia bao la pili dakika ya 56 likifungwa na Alex Iwobi baada ya kazi nzuri ya Alexis Sanchez.
Kwa matokeo hayo Arsenal sasa wanafikisha pointi 13 katika nafasi ya 5 huku Brighton wao wakibaki na pointi zao 7 katika nafasi ya 14.
No comments