YANGA YAFANYA KWELI NJOMBE, YAZOA POINTI ZOTE TATU
Yanga ya Dar es Salaam wakiwa wageni wa Njombe Mji katika uwanja wa Saba Saba mjini Njombe leo hii wamefanikiwa kuibuka na ushindi muhimu mwembamba wa bao 1-0.
Bao pekee la ushindi katika mchezo huo limepatikana katika dakika ya 16 ya mchezo likifungwa na Ibrahim Ajibu kwa mpira wa adhabu uliotinga moja kwa moja wavuni.
Haikua rahisi kwa Yanga kupata ushindi leo kwani Njombe Mji waliisumbua sana ngome yao wakitaka kusawazisha lakini umahiri wa golikipa wa Yanga Youthe Rostand ulimwezesha kuokoa makombora kadhaa yaliyoelekezwa langoni kwake.
Hadi dakika 90 za mchezo huo zinakamilika, Yanga walifanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu ambazo zimewawezesha kufikisha alama nne baada ya kucheza michezo miwili.
Kikosi cha Yanga leo kilikua kama ifuatavyo.
1-Youthe Rostand
2-Juma Abdul
3-Gadiel Michael
4- Andrew Vicent
5-Kelvin Yondani
6-Pappy Tshishimbi
7-Juma mahadhi
8- Thabani Kamusoko/Raphael Daud
9-Donald Ngoma/Obrey Chirwa
10- Ibrahim Ajibu
11- Emmanuel Martine/Yusuf Mhilu
Matokeo mengine katika ligi kuu ya Vodacom leo
Kagera Sugar 1-1 Ruvu Shooting
Lipuli 1-0 Stand United
Singida United 2-1 Mbao FC
Mtibwa Sugar 1-0 Mwadui FC
Mbeya City 0-1 Ndanda FC

No comments