WALICHOKIFANYA MAN CITY NA CHELSEA EPL LEO NI HATARI
Mzunguko wa sita wa ligi kuu nchini England ulianza leo na utakamilika Jumatatu kwa mechi 8 tayari zikiwa zimechezwa leo.
Habari kubwa leo ni ushindi mnono wa Manchester City na Chelsea huku Alvaro Morata akifunga hat-trick katika ushindi wa bao 4-0 walioupata Chelsea dhidi ya Stoke City Ugenini huku goli lingine likifungwa na Pedro.
Manchester City ikiwa nyumbani iliweza kuibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 dhidi ya Crystal Palace ambayo haijawahi kuonja ushindi msimu huu.
Raheem Sterling alifunga mabao mawili,Sergio Aguero,Leroy Sane na Fabian Delph wakifunga bao moja kila moja kuifanya Man City kujiweka vyema katika uongozi wa ligi hiyo ikiwa na magoli mengi.
Manchester United ikiwa ugenini iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Southampton goli pekee la dakika ya 20 la mshambuliaji Romelu Lukaku katika mechi ambayo Man United iliwabidi "kupark bus" kuibuka na ushindi huo kwani Southampton walionekana wako katika ubora wao.
Everton wakiwa nyumbani waliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya AFC Bournemouth. Swansea wakafungwa bao 2-1 nyumbani dhidi ya Watford.
West Ham wakiwa nyumbani wakafungwa bao 3-2 na Tottenham Hotspur wakati Huddersfield wakashindwa kufungana na Burnley.
Mechi ya mwisho leo ilikua baina ya Liverpool dhidi ya wenyeji Leicester City na Liverpool kufanikiwa kushinda kwa bao 3-2 katika mechi ambayo Philipe Coutinho alifunga bao moja na kutengeneza bao moja lililofungwa na Mohammed Salah wakati Nahodha Henderson akifunga bao la tatu.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa King Power ilishuhudia Jermie Vardy akifunga bao moja pamoja na Shinji Okazaki lakini Vardy pia alikosa penati.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa King Power ilishuhudia Jermie Vardy akifunga bao moja pamoja na Shinji Okazaki lakini Vardy pia alikosa penati.

No comments