USHINDI KIDUCHU WAIPA YANGA POINTI 3 MUHIMU

Mabingwa wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara Young Africans imefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda leo katika uwanja wa Uhuru.

Timu zote hazikuonekana kutengeneza nafasi nyingi hali ambayo imeufanya mchezo huo kutokua wa kusisimua.

Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Ibrahim Ajib katika dakika ya 31 kipindi cha kwanza akiunganisha vyema krosi ya Kelvin Yondani

Kwa ushindi huo sasa Yanga wanafikisha pointi 8 baada ya kushuka dimbani mara nne katika ligi kuu ya vodacom.

No comments

Powered by Blogger.