VPL: SIMBA IKO MWANZA KESHO,YANGA DAR JUMAMOSI
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Alhamisi Septemba 21, 2017 kwa mchezo
mmoja utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Katika mchezo huo utakaofanyika kuanzia saa
10.00 jioni utakutanisha timu za Mbao FC ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam.
Utakuwa ni mchezo pekee kwa
siku ya kesho Alhamisi kabla ya ligi hiyo kuendelea Jumamosi ambayo kutakuwa na
michezo minne ambako Young Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Michezo mingine itakuwa ni
Singida United itaialika Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo
utaofanyika Uwanja wa Mwadui ilihali Majimaji itakuwa mwenyeji wa Njombe Mji
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Jumapili Septemba 24, mwaka
huu kutakuwa na michezo mitatu ambako Ruvu Shooting itaialika Mtibwa Sugar
kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani huku Stand United ikicheza na
Mbeya City kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Wakati mechi zote hizo hapo
juu zikianza saa 10.00 jioni, mchezo mwingine siku ya Jumapili utaanza saa 1.00
jioni kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi ukikutanisha Azam na Lipuli ya
Iringa.
No comments