4G YA MAN UNITED YAHAMIA KATIKA KOMBE LA LIGI, CHELSEA YAPIGA MTU MKONO


Mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la ligi nchini England maarufu kama EFL inayodhaminiwa na kampuni ya Carabao Manchester United wameanza vyema kutetea ubingwa wao kwa kuifunga Burton kwa bao 4-1.

Mchezo huo wa hatua ya tatu ulipigwa kwenye dimba la Old Trafford Jijini Manchester huku Marcus Rashford akipiga bao 2 Jesse Lingard na Antony Martial nao wakifunga bao moja kila mmoja kukamilisha ushindi huo wa bao 4 ambao umezoeleka kwa mashabiki wa Manchester United Msimu huu baada ya kushinda mechi za ligi kwa idadi hiyo ya magoli ukiwemo mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Everton.

Mabingwa wa England Chelsea wao walikua nyumbani kucheza na Nottingham Forest na wenyeji Chelsea Kuibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 shujaa wa mchezo ho akiwa ni Michy Batshuayi akifunga hat-trick katika mchezo huo ambao ulishuhudia pia Charly Musonda na Kennedy wakiingia Chelsea mabao yao usiku wa jana.

Katika mechi zingine hiyo jana Everton waliifunga Sunderland bao 3-0, Huku West Brom wakiwa nyumbani wakiambulia kichapo cha bao 2-1 toka kwa Manchester City wakati Arsenal wao wakiwa nyumbani walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 goli pekee la Theo Walcott wakiifunga Doncaster Rovers.

Matokeo ya jana yamezifanya timu hizo kuungana na zingine zilizofuzu juzi kutinga hatua ya 16 bora na tayari ratiba yake imeshatoka 

No comments

Powered by Blogger.