TASWA WALAANI KITENDO CHA OBREY CHIRWA KUMPIGA MWANDISHI
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na wahariri wa habari za michezo nchini wametoa tamko kwamba wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kushambuliwa kwa mwanahabari John Dande, zinazodaiwa kufanywa na straika wa Yanga, Obrey Chirwa, siku ya Jumanne katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
TASWA na wahariri wa habari za michezo, wamelaani tukio hilo la kushambuliwa kwa Dande ambaye ni mpigapicha wa Kampuni ya New Habari 2006 Limited, kwani kitendo hicho si cha kiungwana bali ni udhalilishaji wa taaluma ya habari na hujuma kwa tasnia.
Kwa sababu ambazo hazijafahamika, Obrey Chirwa anadaiwa kumshambulia mwanahabari huyo akiwa katika majukumu yake kwenye uwanja wa Uhuru wakati Yanga wakiwa mazoezini.
Tayari tukio hilo limeripotiwa polisi.
mpira umemshinda au anatafuta sababu ya kuondoka nchini?
ReplyDelete