TAMBWE NA KESSY WAANZA MAZOEZI YANGA
Wachezaji wa Yanga Amisi Tambwe na Hassan Kessy ambao walikua wakisumbuliwa na majeraha wamepona na kurejea katika kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa kesho katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Tambwe aliyekua akisumbuliwa na goti kwa muda mrefu amerejea huku akianza kwa kufanya mazoezi ya peke yake, hali inayoonesha kwamba hana nafasi kubwa ya kucheza katika mchezo huo wa kesho.
Naye Kessy ambaye alikua akisumbuliwa na majeraha aliyoyapata katika ajali ya pikipiki juma lililopita, amerejea kwenye mazoezi mepesi huku naye pia akionekana kutokua na dalili za kuhusika katika mchezo huo.
No comments