MESSI APIGA HAT-TRICK BARCELONA IKIENDELEZA USHINDI 100% LA LIGA


Klabu ya Barcelona jana iliendeleza wimbi la ushindi msimu huu ikipata ushindi wa tatu mfululizo tangu kuanza kwa msimu huu.

Lionel Messi alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa bao 5-0 walioupata nyumbani jana dhidi ya Espanyol.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika tayari Barcelona walishafunga mabao mawili yote yakiwekwa kimiani na Lionel Messi dakika za 26 na 35 halafu akaongeza bao la tatu dakika ya 67 katika mechi ambayo  Gerard Pique na Luis Suarez pia walifunga bao moja kila mmoja.

Matokeo ya jana yanaipaisha Barcelona kileleni ikifikisha pointi 9 katika nafasi ya kwanza ikiwa ndiyo timu pekee pamoja na Real Sociedad ambazo hazijapata sare wala kufungwa tangu msimu huu uanze lakini Sociedad wao wamecheza michezo miwili tu.

No comments

Powered by Blogger.