MAN CITY YAFUNIKA KWA PESA NYINGI USAJILI ENGLAND
Manchester City imeongoza kwa matumizi ya pesa kwenye dirisha la usajili la majira ya joto ambalo limefungwa mwishoni mwa mwezi Agosti.
Hesabu zinaonesha City wametumia £134.1 milioni Inafahamika kwamba Man City walilazimika kutumia £226.7 milioni kununua mastaa kadhaa lakini wao waliingiza £92.6 milioni kwa kuuza wachezaji wake. Hivyo hesabu inaonesha £134.1 milioni ndiyo pesa iliyowayoka.
Kwa hesabu ya aina hiyo, inaonesha Tottenham wametumia pesa ndogo zaidi ukilinganisha na timu nyingine sita za juu katika ligi kuu ya England.
Walitumia £101.8 milioni kununua wachezaji kisha wakauza wachezaji wenye thamani ya £90.3 milioni hivyo gharama halisi waliyotumia ni £11.5 milioni
Kocha anaefahamika kwa Ubahili, Arsene Wenger wa Arsenal yeye ametumia £14.3 Milioni. Alimpata beki Sead Kolasinac bure kabla ya kumsajili Alexandre Lacazette kwa £46.5 milioni.
Everton walitumia £46.2 milioni, Liverpool £50.3 milioni akinunua kwa £84.9 na kuuza kwa £34.6.
Chelsea walitumia £75.7 milioni huku Man UTD wao wakitumia £140.7 milioni kununua wachezaji na kuingiza £10 milioni kwenye mauzo. Hivyo wametumia £130.7

No comments