LUKAKU AIPELEKA MAPEMA UBELGIJI KOMBE LA DUNIA

Wachezaji wa Ubelgiji wakishangilia bao la kwanza

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji na klabu ya Manchester United Romelu Lukaku ameibuka kuwa shujaa kwa nchi yake baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Ugiriki katika mechi za kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia mwakani nchini Russia.

Ikicheza ugenini Ubelgiji ilitangulia kupata bao kupitia kwa beki wake anayeichezea Tottenham Jan Vertonghen kabla ya Ugiriki hawajasawazisha kupitia kwa Zeca dakika ya 73 ya mchezo ikiwa ni dakika 3 tu tangu Vertonghen alipofunga lakini Lukaku akapigilia msumari wa mwisho akifunga bao la ushindi dakika 1 baadae.

Ushindi huo unaifanya Ubelgiji kuwa timu ya kwanza kukata tiketi kwa bara la Ulaya ukiacha wenyeji Russia wakifikisha pointi 22 kwenye Group H ambazo haziwezi kufikiwa na nchi yoyote.

No comments

Powered by Blogger.