HII NDIYO SABABU ILIYOZUIA COUTINHO KUSAJILIWA NA BARCELONA

Siku chache baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili barani Ulaya hususani nchini England klabu ya Barcelona imetoa sababu za kwanini walishindwa kumsajili Philipe Countinho kutoka Liverpool.

Barcelona imedai kwamba Liverpool ilihitaji ilipwe paundi milioni 183 ili iweze kumruhusu mchezaji huyo nyota wa Brazil kutimkia jijini Barcelona ikiwa ni siku ya mwisho ya kufungwa kwa dirisha la usajili na hii imesemwa na Mkurugenzi wa Barcelona Albert Soler.
Liverpool wamekataa maombi matatu kutoka kwa mabingwa hao wa zamani wa  Uhispania kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikuwa ameomba uhamisho.
Soler ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano na wanahabari siku ya Jumamosi aliongezea: Hali ilimalizika ilivyomalizika na hakuna chengine tunachoweza kufanya.
Barcelona ilimtaka Coutinho baada ya kumuuza Neymar kwa PSG kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha £200m.
Liverpool imesema kuwa Coutinho hauzwi na kukataa maombi ya £72m, £90m na jingine la £114m kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho nchini Hispania ambalo lilifungwa siku moja baada ya lile la Uingereza kufungwa.

No comments

Powered by Blogger.