KWA MAAMUZI HAYA YA PERISIC BASI MAN UNITED WASAHAU KUMSAJILI


Mmoja kati ya wachezaji waliozungumzwa sana kusajiliwa na Manchester United Ivan Perisic ambaye uhamisho wake kutoka  Inter Milan ulikwama kutokana na klabu hizo kutofikia makubaliano ameamua kusaini mkataba mpya.

Ivan Perisic winga wa kimataifa wa Croatia mwenye miaka 28 amesaini mkataba mpya wa miaka mitano kuichezea Inter Milan.

Man United itabidi isahau kumsajili mchezaji huyo kwa bei ya kawaida sasa baada ya mkataba huu mpya wa miaka mitano ambao utamweka klabu ni hapo mpaka msimu wa 2021/2022.


No comments

Powered by Blogger.