AZAM FC VS SIMBA SC SASA KUPIGWA JIONI BADALA YA USIKU


Pambano la ligi kuu ya soka Tanzania bara baina ya miamba miwili jijini Dar es Salaam Azam FC na Simba SC limerudishwa saa 10 alasiri baada ya saa moja jioni.

Sababu kubwa ya kurudisha pambano hilo nyuma ni maswala ya usalama na tayari timu zote zimeshatarifiwa yani wenyeji Azam Fc na Wekundu wa Msimbazi Simba.

Hii ni mechi ya kwanza katika historia ya ligi kuu soka Tanzania bara kuchezwa kwenye dimba la Chamazi (Azam Complex) ikizihusisha Azam FC dhidi ya wakongwe wa Soka nchini Simba na Yanga.

Mwamuzi wa mchezo huo anabaki yule yule Ludovick Charles wa Tabora akisaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Abdallah Mkomwa wa Pwani wakati Mezani atakua Josephat Bulali na kamisaa ni Ruvu Kiwanga wote toka Dar es salaam na viingilio vinabaki kama vilivyokua mwanzo 7,000 mzunguko na 10,000 kwa VIP.

1 comment:

Powered by Blogger.