HAPATOSHI LIGI YA MABINGWA ULAYA LEO: RATIBA YOTE HII HAPA


Hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya inaanza leo kwa mechi 8 kuchezwa katika viwanja tofauti barani humo.

Moja kati ya mechi inayotazimiwa kutazamwa sana ni baina ya wenyeji Barcelona na Juventus ikiwa ni moja ya mechi mbili katika kundi D.
Mechi hiyo ni kama marudio ya mechi ya hatua ya nusu fainali msimu uliopita ambapo Juventus iliweza kuibuka na ushindi wa jumla.

Mechi nyingine  itazikutanisha Sporting Lisbon ya Ureno itakayosafiri kuivaa Olympiacos ya Ugiriki.

Kundi A pia litashuhudia Manchester United wakiwa Nyumbani kuwaalika FC Basel kutoka Uswisi huku Benfica ya Ureno ikimenyana na CSKA Moscow.

Kundi B matajiri PSG watasafiri kuivaa Celtic ya Scotland mechi itakayotoa mwangaza wa usajili wa paundi zaidi ya milioni 300 walizotumia PSG wakati kwenye mechi nyingine ya kundi hilo Bayern Munich watakua nyumbani kuialika Anderletch kutoka Ubelgiji.

Kundi C Mabingwa wa England Chelsea watakua nyumbani kuialika Qarabag FK ya Azerbaijan wakati AS Roma wao watawaalika Atletico Madrid toka Spain.

Mechi zote hizi zitaanza majira ya saa 4 kasorobo kwa saa za hapa nyumbani Afrika Mashariki huku mechi zingine 8 zikitarajiwa kuchezwa kesho Jumatano.

No comments

Powered by Blogger.