DIEGO SIMEONE AJIFUNGA KIMKATABA ATLETICO MADRID


Kocha mkuu wa Atletico Madrid Diego Simeone ameongeza mkataba wake wa kuifundisha Atletico Madrid kwa miaka mitatu zaidi.

Simeone ambaye anatimiza mwaka wa saba sasa akiwa kama kocha wa klabu hiyo akisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na kufuta matumaini ya Inter Milan waliokuwa wanamwania.

Kocha huyo mwenye miaka 47 amesaini mkataba mpya utakaomweka mpaka mwaka 2020 huku mkataba wake wa awali ulikua ukimalizika baada ya msimu ujao.

Simeone akiwa na Atletico Madrid ameweza kupata mafanikio mbele ya wababe wa laliga akishinda La Liga mara moja,Copa del rey, Spanish Super Cup,Uefa Super cup na Europa league.

No comments

Powered by Blogger.