ARSENAL YASHANGAZA MASHABIKI WAKE TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI
Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki wa Arsenal wameonekana kushangazwa na uteuzi wa mlinzi wao mpya Sead Kolasinac kama mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi Agosti.
Mashabiki wengi wa Arsenal katika Ukurasa wa Twitter baada ya kutolewa habari kwamba Kolasinac ameshinda tuzo hiyo walijibu kwa mshangao mkubwa kuhusu kigezo kilichotumika kumpa mchezaji huyo.
Ndani ya Mwezi Agosti Arsenal ilicheza mechi 3 ikishinda moja sare moja na kupoteza moja huku Kolasinac akicheza mechi moja dakika zote 90 yani dhidi ya Leicester City huku akitolewa kwenye mechi ya sare dhidi ya Stoke na hakupangwa kabisa wakati kikosi cha Wenger kilipofungwa bao 4-0 na Liverpool.
Katika tuzo hizo Beki huyo amepata 50% akiwashinda Alexandre Lacazette aliyepata 26% na kipa Petr Cech aliyepata 25%.
NINI MAONI YAKO?

No comments