BAADA YA SHUGHULI PEVU MKOANI YANGA LEO IKO DAR.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Jumamosi Septemba 23, kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.
Mabingwa watetezi Young Africans maarufu kama Yanga baada ya michezo miwili mikoani na kuambulia pointi 4 inarejea tena Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa nne kwenye ligi dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Ikumbukwe Yanga ilianza Ligi kwa sare katika uwanja huo huo wa Uhuru dhidi ya Lipuli FC toka Iringa na leo itakua na kazi nyingine dhidi ya Ndanda FC timu inayoonekana kuwa na upinzani mkali inapocheza ugenini ikichagizwa na pointi 4 ambazo wamezipata jijini Mbeya dhidi ya Mbeya FC na Prisons.
Huko Mkoani Shinyanga katika migodi ya Madini ya Mwadui Wakongwe katika soka la Tanzania Mwadui FC watawakaribisha maafande wa Prisons toka jijini Mbeya katika Uwanja wa Mwadui.
Mchezo mwingine, utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea Ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Njombe Mji bila ya kocha wake Ahmed Hassan Banyai aliyebwaga manyanga wakati Maji maji wao wakiwa na moto ule waliouwasha dhidi ya Yanga na kupata sare ya bao 1-1.
Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.

No comments