YANGA "YATESTI MITAMBO" KWA MORO KIDS, YAWASHUSHIA MVUA YA MAGOLI
Klabu ya Yanga iliyopo Kambini Morogoro, asubuhi ya leo ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Moro Kids katika uwanja wa seminari, Bigwa.
Katika mchezo huo wa kutesti mitambo, Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 huku wakiwajaribu wachezaji wao wote waliopo katika kambi hiyo isipokua Geofrey Mwashiuya na Obrey Chirwa ambao wamepata majeraha.
Katika ushindi huo, mabao ya Yanga yalifungwa na Donald Ngoma aliyefunga mawili, Amisi Tambwe aliyefunga bao moja huku Yusuf Mhilu na ingizo jipya Raphael Daudi nao wakifunga bao moja moja.
Yanga wameweka kambi katika hoteli ya B-Z iliyopo Nane-Nane Morogoro.

No comments