RASMI : HARUNA NIYONZIMA KUICHEZEA SIMBA MSIMU UJAO

Hatimaye klabu ya Simba imethibitisha kumsajili kiungo mahiri raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima kutoka Yanga ambako amemaliza mkataba.

Uthibitisho huo umetolewa na msemaji mkuu wa klabu hiyo, Haji Manara alipoulizwa kuhusu usajili wa kiungo hiyo. Haji amesema tayari wamemalizana na Haruna na atatua nchini hivi karibuni baada ya kumaliza majukumu yake binafsi ya kifamilia huko nchini kwao.

"Kuhusu Haruna ni mchezaji wa Simba ukiona ndege imetua hapa na wachezaji wa Simba ujue ndani yupo Haruna au anaweza kuja mapema kabla ya timu" alisema Haji.

Kikosi cha Simba kipo nchini Afrika Kusini kwa maandalizi ya ligi na mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda utakaopigwa kwenye tamasha la Simba Day Agosti 8 mwaka huu katika uwanja wa taifa.

Simba hutumia tamasha hilo kutambulisha wachezaji wapya, hivyo huenda Haruna akatambulishwa pia siku hiyo.

No comments

Powered by Blogger.