WENGER AMNG'ANG'ANIA SANCHEZ KWA LAZIMA, APINGANA NA BODI

Sanchez suffered an abdominal strain during a training session and will miss two matches
Inaripotiwa kua baadhi ya wakurugenzi wa Bodi ya Arsenal wamekua wakisisitiza ikija ofa ya zaidi paundi milion 50 kwa Alexis Sanches basi Mchezaji huyo auzwe bila kujali ni klabu gani inamtaka.

Lakini taarifa zinasema Arsene Wenger ameshikilia msimamo wa kumbakiza mchezaji huyo ata kama ni kumpoteza bure msimu ujao.

Bodi inaripotiwa kukubaliana na mawazo hayo kwa shingo upande huku Arsene Wenger akiendelea kupambania dili la kumsajili Tomas Lemar kutoka Monaco.

Lakini bodi inakataa kutoa zaidi ya fedha zinazotakiwa na Monaco, ikisisitiza ni lazima Arsenal ipunguze kwanza baadhi ya wachezaji ambao hawaitajiki kama Debuchy, Gibbs, Perez na Jenkinson.

No comments

Powered by Blogger.