WAYNE ROONEY AENDELEA KUITESA MAN CITY LIGI KUU YA ENGLAND


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United anayeichezea Everton hivi sasa Wayne Rooney ameendelea kuitesa Manchester City akifunga bao moja lililowapa Everton pointi moja ugenini.

Wakicheza mchezo wa mwisho wa raundi ya pili ya msimu mpya katika ligi kuu ya England kwenye dimba la Etihad Man City na Everton zilitoshana nguvu na kwenda sare ya kufungana bao 1-1.

Wayne Rooney ndiye aliyetangulia kuifungia Everton bao la kwanza likiwa ni bao lake la 200 katika ligi kuu ya England akiwa ndiye mchezaji wa pili katika historia ya ligi hiyo kufikisha mabao 200 au zaidi wa kwanza akiwa ni Allan Shearer na bao la kusawazisha la Man City likifungwa na Raheem Sterling.

Kwenye mchezo huo wachezaji wawili walipata kadi nyekundu kwa makosa tofauti Kyle Walker wa Man City kipindi cha kwanza na Morgan Schneiderlin wa Everton kuzifanya timu hizo kufikisha pointi 4 kila moja.

No comments

Powered by Blogger.