SIMBA YATEST MITAMBO SIMBA DAY,NIYONZIMA OKWI NA KICHUYA WAACHA GUMZO

Mohammed Ibrahim akipongezwa na wachezaji wenzake
Wawakilishi wa Tanzania bara kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika Wekundu wa Msimbazi Simba leo wamefungua msimu mpya wa ligi na michuano mbalimbali kwa kucheza mechi dhidi ya Mabingwa wa Rwanda klabu ya Rayon Sports.

Pambano hilo ambalo lilikua ni kilele cha wiki ya simba na kuitwa Simba Day lilichezwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar ambapo Wekundu hao waliwalaza Rayon kwa bao 1-0.

Kazi nzuri ya Emmanuel Okwi ilizaa bao lililofungwa na Mohammed Ibrahim bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo licha ya kosa kosa nyingi katika lango la Rayon.

Kivutio kwenye mchezo wa leo alikua Shiza Kichuya ambaye alionyesha uwezo mkubwa huku Emmanuel Okwi naye akiwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Rayon na hata alipoingia Haruna Niyonzima alionyesha kabisa kwanini Simba walikomaa kumsajili.

Simba ilitumia mchezo wa leo kutambulisha wachezaji wake wapya na kutambulisha jezi mpya za msimu mpya katika uwanja wa Taifa ambao ulifurika mashabiki wa Simba.

No comments

Powered by Blogger.