REAL MADRID YAINYUKA MAN UNITED N KUTWAA UBINGWA WA SUPER CUP
Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wametwaa ubingwa wa Super Cup baada ya kuifunga Manchester United bao 2-1 katika mchezo uliowashirikisha Real Madrid kama mabingwa ligi ya mabingwa Ulaya na Manchester United kama mabingwa wa Europa League.
Mchezo huo ni ufunguzi rasmi wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya msimu mpya wa mwaka 2017/2018 ambao umeshaanza hatua ya mtoano.
Uzembe wa mabeki waMan United hasa Antonio Valencia ya kudhani wafungaji walikua wameotea ulipelekea Casemiro na Isco kuipatia Madria mabao muhimu huku Romelu Lukaku akifunga bao pekee la Manchester United usiku huu.
Licha ya matokeo hayo pande zote mbili zilikosa magoli ya wazi huku Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mchezaji bora wa dunia kwa sasa akiingia dakika za mwisho na kushindwa kuonyesha makeke yake.
No comments