SIMBA YATAFUNA MIWA YA MTIBWA BAADA YA MKUTANO MKUU,OKWI ATUPIA


Wekundu wa Msimbazi Simba wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ngumu ya Mtibwa Sugar toka Mkoani Morogoro.

Shukrani za dhati kwa Emmanuel Okwi ambaye ndiye aliyefunga bao pekee la Simba leo akifunga bao hilo kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Mchezo huo ulikua ni wa kirafiki kujiandaa na msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.

Kabla ya Mchezo wa leo Simba ilifanya mkutano wake mkuu wa mwaka katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam ambapo mambo kibao yalipitishwa na maadhimio mengi yaliungwa mkono likiwemo la kufukuzwa uanachama kwa aliyekua mjumbe wa bodi ya wadhamini wa klabu hiyo Mzee Hamis Kilomoni.

No comments

Powered by Blogger.