LUKAKU APIGA 2 MAN UNITTED IKISHINDA 4-0, SPURS NAYO YAIKANDAMIZA NEWCASTLE


Mabingwa wa Europa League Manchester United wameanza vyema kinyang'anyiro cha ligi kuu ya England kwa kuifunga West Ham United bao 4-0.

Man United ilionekana iko njema zaidi hasa eneo la kiungo likiongozwa na Nemanja Matic mchezaji mgeni katika kikosi hicho aliyesajiliwa akitokea Chelsea.

Romelu Lukaku aliipatia Man United bao la kwanza kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko huku United ikikosa nafasi nyingi.

Kipindi cha Pili Man United waliongeza kasi na ufundi zaidi na kupelekea kupata bao la Pili lililofungwa na Romelu Lukaku kisha Paul Pogba na Antony Martial nao wakifunga bao moja kila mmoja.

Ushindi huo unaifanya Man United kuongoza ligi hiyo baada ya mechi za kwanza ikiwa ndiyo timu pekee iliyofunga magoli mengi bila kuruhusu kufungwa.

Katika mechi ya mapema leo Wageni kwenye ligi kuu Newcastle walikaribishwa kwa kufungwa bao 2-0 na Tottenham Hotspur magoli ya Delle Alli na Ben Davies.

No comments

Powered by Blogger.