SIMBA YAMALIZA MECHI ZA MAJARIBIO "SAUZI" KWA SARE


Wawakilishi wa Tanzania katika kombe la shirikisho barani Afrika Wekundu wa Msimbazi Simba wamemaliza Ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara na michuano mingine kwa kwenda Sare na mabingwa wa Soka Afrika Kusini klabu ya Bidvest Vits ya huko 

Simba iko Nchini Afrika Kusini kwa wiki ya Pili sasa ikijiandaa na msimu mpya na leo asubuhi ilicheza mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Bidvest na kutoka sare ya bao 1-1 ikiwa ni mechi ya pili ya kujipima nguvu 

Juzi katika mechi yao ya Kwanza Simba ilifungwa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates ya huko huko Afrika Kusini moja kati ya timu kongwe na maarufu kwenye ligi ya Afrika Kusini maarfu kama Premier Soccer League (PSL)

Weekend hii kikosi cha Simba kitarejea nchini tayari kwaajili ya mechi yao ya Siku ya Simba (Simba Day) siku ya nane nane kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar ambapo Simba itacheza dhidi ya Rayon Sport toka Nchini Rwanda kabla ya kuivaa Yanga kwenye mechi ya Ngao ya Jamii wikiend ijayo baada ya Simba Day. 

No comments

Powered by Blogger.