SIMBA KUJIPIMA NA MLANDEGE LEO USIKU



Wekundu wa msimbazi Simba wataingia dimbani usiku wa leo majira ya saa 2 kamili usiku kucheza mchezo wa kwanza wa kirafiki kisiwani Unguja dhidi ya Mlandege ya huko.

Mchezo huo ni wa kujipima nguvu kabla ya kucheza na Yanga Jumatano Ijayo pia ni moja ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza wiki ijayo 

Simba iko Visiwani zanzibar wakati watani zao Yanga wao wako Pemba ambako wameweka kambi ya mazoezi kujiandaa na mchezo huo na kujiweka tayari kwaajili ya ligi kuu Tanzania bara na michuano ya kimataifa.

No comments

Powered by Blogger.