SERIKALI YAKUBALI MABADILIKO KATIKA KLABU YA SIMBA ~ DR. KIGWANGALA


Mgeni Rasmi wa mkutano mkuu wa klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam unaoendelea hivi sasa Mheshimiwa Naibu Wazir wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia na watoto Mheshimiwa Dr.Hamis Kigwangala ameridhia mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya hiyo kongwe nchini.

Dr.Kigwangala ameonyesha kufurahia mabadiliko yaliyopitishwa na klabu hiyo huku akisema serikali inaunga mkono mabadiliko ya mfumo ambao utapelekea mabadiliko si tu katika utendaji bali katika uchumi pia ambayo ni maendeleo kwa Taifa.

Aidha Dr. Kigwangala amewashukuru viongozi wote wa Simba hasa kamati ya mabadiliko ambayo ilijitahidi kutoa elimu kwa kila mwana Simba Hakika majina yao yatabaki milele na kuandikwa kwa wino wa dhahabu.

"Nilisoma na kujiridhisha kilichoandaliwa na wataalamu kuhusu mabadiliko kwani mimi ni mmoja wa watu ambao mwanzoni hatukuelewa swala hili na kujua kua klabu inaunga lakini sasa kila mmoja anajua umuhimu wa mabadiliko haya"

"Kwa muundo huu uchumi wa klabu utaimarika, uchumi wa wanachama utaimarika, maslahi ya wachezaji yataboreshwa na daima itasaidia kuweka msingi bora wa mafanikio"

"Jina la Simba ni kubwa Afrika lakini mafanikio hayaendani na ukubwa wa jina hilo kupelekea kushindwa kushinda na vilabu kama TP Mazembe, Al Ahly n.k sasa ni wakati mzuri wa kuanza kutamba Afrika baada ya mabadiliko haya"

Aidha Dr. Kigwangala ameeleza jinsi serikali iliyoko madarakani ioivyopania kuboresha michezo nchini kwa kukarabati viwanja na kukaribisha uwekezaji wa ujenzi wa uwanja mpya mjini Dodoma.

Mkutano wa leo kwa kauli moja umepitisha mabadiliko kutoka kwenye mfumo wa awali kwenda katika mfumo wa hisa

No comments

Powered by Blogger.