ALICHOSEMA MAKAMU RAIS WA TFF MICHAEL WAMBURA KWENYE KIKAO CHA MABADILIKO YA SIMBA SC
Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF Michael Richard Wambura ni mmoja kati ya wageni waalikwa kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam mkutano unaoendelea hivi sasa katika ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Nyerere.
Wambura mmoja kati ya watu waliopigwa vita sana alipotaka kugombea katika uongozi wa klabu ya Simba na kupelekea kufukuzwa uanachama leo ameonekana kama shujaa akishangiliwa na wanachama zaidi ya elfu moja walioujaza ukumbi huo wenye hadhi ya kimataifa.
Aidha Wambura kwenye mkutano huu ameelezea umuhimu wa mabadiliko ya uendeshaji kutoka katika kuwa na klabu inayojiendesha kwa kujifurahisha tu kwenda kwenye klabu itakayompa mwanacahama kipato lakini pia kuhakikisha klabu inasonga mbele kwa ufanisi mkubwa.
"Ni vizuri kuthubutu wakati huu ambao wengi wetu hatuna aina yoyote ya uwekezaji lakini kwa sasa baada ya mabaodiliko kila mwanachama ataweza kupata faida ya kuwa si tu mwanachama wa Simba"
"Ni muda sasa kwa wale makomandoo wanaokaa Milangoni kuzuia mapato kwa maslahi yao kwani sasa watakua wanajidhulumu wenyewe kwani wao ni kati ya wamiliki wa Simba"
"Ni vyema vilabu vingine vikaiga mfumo huu kwa maendeleo ya soka letu na nawasihi kuboresha umoja wetu ili kufikia mabadiliko ya kweli na Hakika siku moja tutakua mabingwa wa Afrika".
Hayo ndiyo aliyoyasema Michael Wambura na mkutano unaendelea muda huu
No comments