REAL MADRID YAIADHIBU TENA BARCELONA NA KUTWAA UBINGWA WA SUPER CUP SPAIN
Mabingwa wa Ulaya na La Liga Real Madrid wameendeleza ubabe wao dhidi ya Barcelona baada ya kuifunga tena kwenye mchezo wa pili wa Super Cup nchini Hispania.
Real Madrid imeibuka na ushindi wa bao 2-0 katika mechi iliyomalizika muda mfupi uliopita na kutwaa ubingwa wa kombe hilo ambalo ni la ufunguzi wa msimu mpya wa La Liga kwa ushindi wa jumla wa bao 5-1.
Marco Asensio na Karim Benzema walifunga mabao mawili hayo ya Real Madrid katika mchezo ambao Kocha wa Real Madrid Zenedine Zidane licha ya kumkosa Cristiano Ronaldo aliwaweka nje pia Gareth Bale na Isco ambao wamekua mhimili mkuu wa Real Madrid katika siku za hivi karibuni.
No comments