REAL MADRID VS BARCELONA KURUDIANA LEO USIKU MNENE


Mechi ya El Clasico ambayo ni ya marudiano katika Super Cup ya Hispania baina ya mabingwa wa La Liga Real Madrid dhidi ya mabingwa wa Copa del rey Barcelona inatazamiwa kuchezwa usiku wa leo katika dimba la Santiago Bernabeu.

Mechi hiyo itaamua timu ipi itatwaa ubingwa huo ambao huashiria ufunguzi wa ligi kuu ya Spain La Liga kwa msimu wa mwaka 2017/2018 unaotazamiwa kuanza wikiend hii.

Katika mechi ya awali iliyopigwa Jumapili Barcelona ikiwa nyumbani ilikubali kichapo cha bao 3-1 lakini kwenye mechi ya leo Real Madrid watamkosa Cristiano Ronaldo ambaye amefungiwa mechi 5 kufuatia kumsukuma mwamuzi kwenye mchezo uliopita.

Mechi hii ya leo itaanza majira ya saa 6 kamili za Usiku kwa saa za hapa nyumbani.

No comments

Powered by Blogger.