RASMI : WAYNE ROONEY AAMUA KUSTAAFU SOKA LA KIMATAIFA
Wayne Rooney ametangaza kustaafu kuchezea Timu ya Taifa ya England ikiwa ni miaka 14 tangu alipoitwa kuichezea kwa mara ya kwanza mwaka 2003.
Akiwa na miaka 31 hivi sasa Rooney ameamua kuachana na soka la kimataifa ili kujipa muda kuitumikia klabu yake pendwa ya Everton ambayo amerejea kuichezea msimu huu.
Kulikua na tetesi za pengine angeitwa na kocha Gareth Southgate baada ya kuanza vyema akiwa na Everton akifunga tayari bao mbili mpaka sasa katika mechi mbili.
Anastaafu kwa heshima kubwa akiwa ndiye mchezaji aliyyefunga magoli mengi zaidi kwa timu ya taifa ya England akiwa amefunga mabao 53 katika michezo 119 aliyoweza kuichezea.
No comments