MWISHO WA "WAVUTA BANGI" LIGI KUU TANZANIA BARA UMEWADIA

Image result for LIGI KUU TANZANIA BARA
Shirikisho la soka Tanzania TFF linataraji kupiga hatua muhimu katika soka la ueledi kulingana na maendeleo ya mchezo huo pendwa duniani. Hatua hiyo ni ile ya kupiga vita matumizi ya dawa zisizofaa michezoni, kampeni ambayo imekua ikiendeshwa na vyama vyote vya michezo duniani.

Akiongea na wanahabari jana, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema wanataraji kuanzisha utaratibu wa kuchukua vipimo vya wachezaji katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom unaotarajiwa kuzinduliwa kesho katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Alfred amesema kwa kuanzia, wachezaji wa Simba na Yanga watachukuliwa sampuli kwa ajili ya vipimo hivyo kesho na zoezi hilo litaendelea katika michezo mingine ya ligi.

Hata hivyo Alfred aliweka wazi kwamba hatua hiyo haimaanishi kwamba wana hofu kuwa baadhi ya wachezaji wa timu fulani wanatumia dawa hizo, bali ni katika kuhakikisha kuwa soka inabaki kuwa mchezo wa kistaarabu 'fair play'.

No comments

Powered by Blogger.