RASMI ; NEYMAR AKAMILISHA UHAMISHO WAKE KUELEKEA PSG

Neymar has signed for Paris Saint-Germain on a five-year contract from Barcelona
Dunia imeshuhudia rekodi mpya na ya kipekee ikiwekwa na kijana wa Brazil mwenye miaka 25 tu Neymar Da Silva akisaini mkataba wa miaka mitano kuichezea PSG kwa ada ya uhamisho paundi milioni 198 akitokea Barcelona.

Wanasheria wake Neymar jana walifika kwenye ofisi za Shirikisho la Soka la Hispania kupeleka hundi ya malipo ya kuvunja mkataba wa mchezaji huyo lakini ilikataliwa na ndipo wakaamua kuipeleka kwenye klabu ya Barcelona ambao waliipokea na kukamisha uvunjaji wa mkataba wa mchezaji huyo.

Tofauti na uhamisho wa wachezaji wengine unavyofanyika ambapo klabu na klabu zinakubaliana lakini uhamisho wa Neymar umemuhusisha yeye mwenyewe kupitia kwa wanasheria wake ili kuiepusha PSG kukumbana na rungu la Uefa kuhusu sheria ya matumizi ya fedha michezoni (Financial Fair Play)

Neymar amesaini mkataba wa miaka mitano na atakua akilipwa kiasi cha paundi karibia laki 5 kwa wiki na kumfanya ndiye mchezaji ghali zaidi duniani kwa uhamisho akivunja rekodi ya Paul Pogba.

No comments

Powered by Blogger.