LACAZETTE AWEKA REKODI ARSENAL IKIFUNGUA LIGI KWA USHINDI DHIDI YA LEICESTER CITY
Ilimchukua dakika mbili tu mshambuliaji mpya wa timu hiyo Alexandre Lacazette kufunga bao la kwanza ambalo linamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika msimu mpya wa ligi kuu ya England 2017/2018.
Licha ya Ushindi huo lakini haikua kazi rahisi kwa Arsenal kuupata kwani Leicester City walionekana kuimarika vilivyo na kuisumbua sana Arsenal wakifunga mabao yao kupitia kwa Shinji Okazaki na magoli mawili ya Jarmie Vardy huku Danny Welbeck,Aaron Ramsey na Oliver Giroud.
Ligi hiyo itaendelea tena leo kwa mechi ya kwanza saa 8 na nusu kati ya Watford na Liverpool huku mechi ya mwisho ikiwa kati ya Brighton na Manchester City huku kukiwa pia na mechi zingine nyingi zikipigwa saa 11.
No comments