DANGOTE AJITOSA TENA KUTAKA KUINUNUA ARSENAL NA KUAHIDI KUMTIMUA WENGER
Mmoja kati ya mabilionea Katika bara la Afrika Mnigeria Aliko Dangote ameonyesha tena dhamira yake ya kutaka kuinunua Arsenal ya England na kuahidi iwapo atauziwa basi atamfungashia virago Kocha Arsene Wenger ambaye hana dalili za kuondoka klabuni hapo kwasasa.
Akizungumza na mtandao wa biashara wa Bloomburg Dangote ambaye anamiliki visima vya mafuta Nchini Nigeria lakini pia akijitanua kwa biashara mbalimbali Afrika ikiwemo biashara ya Cement ambapo Tanzania ni moja ya nchi zinazonufaika na uwekezaji wake amesema "Nikiipata Arsenal kitu cha kwanza ni kuhakikisha Arsene Wenger anaondoka klabuni, Amefanya mambo mengi lakini ni muda muafaka wa kumwachia mwingine kujaribu bahati yake"
Dangote ni Mmoja wa mashabiki "lia lia" wa Arsenal na kwa muda mrefu amekua akionyesha dhamira ya kutaka kuinunua klabu hiyo inayomilikiwa na Bilionea Stan Kroenke ambaye ameshaweka wazi kuwa Arsenal haiuzwi kwa gharama yoyote ile.
No comments