BARCELONA YAMNASA DEMBELE WA DORTMUND KWA DAU LA KUFURU


Borussia Dortmund imekubali kumuuza mshambuliaji wake Raia wa Ufaransa Ousmane Dembele kwenda klabu ya Barcelona kwa ada ya uhamisho paundi milioni 135.5.
Mchezaji huyo mwenye miaka 20 bei yake ilikua Paundi milioni 11 tu msimu uliopita lakini bei hiyo imepanda zaidi maradufu msimu huu kutokana na mabadiliko katika soko la wachezaji kwasasa duniani.

Dembele anakua mchezaji wa pili ghali duniani baada ya Neymar ambaye wiki chache zilizopita alinunuliwa na PSG akitokea Barcelona.

Barca wamelipa pesa taslimu paundi milioni 96.8 ambayo itaongezeka mpaka kufikia paundi milioni 135.5 kutokana na ushiriki wa mchezaji huyo katika ligi ya mabingwa Ulaya na mafanikio mengine akiwa na Barcelona na amesaini mkataba wa miaka mitano atavaa jezi namba 11 na kufanyiwa vipimo vya afya Jumatatu.

No comments

Powered by Blogger.