WENGER AWEKA KANDO UBAHIRI, AMSAJILI LACAZETTE KWA PESA NDEFU
Klabu ya Arsenal jana Ilikamisha uhamisho wa Mshambuliaji Alexandre Lacazette kwa Ada ya Uhamisho wa kihistoria katika klabu hiyo wa paundi milioni 53 akitokea Olimpic Lyon ya Ufaransa.
Msambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu alikua jijini London tangu Jumanne kwaajili ya vipimo vya afya kusaini mkataba na kukamilisha uhamisho huo.
Lacazette amesaini mkataba wa miaka miatano kuichezea Arsenal ambao ni mabingwa wa Kombe la FA.
Huu ni uhamisho wa kwanza mkubwa kwa klabu hiyo ukivunja rekodi ya Uhamisho wa mesuit Ozil wa paundi milion 42.5 mwaka 2013.
Lyon wamepata kiasi cha paundi milioni 46 taslimu huku paundi milioni 7 zitalipwa na Arsenal kutokana na maendeleo ya mchezaji.
lacazette mwenye miaka 26 ameifungia lyon mabao 136 katika mechi 289 na ujio wake pengine ukafanya mshambuliaji Olivier giroud aondoke klabuni hapo West ham na Everton wakimtolea macho.
No comments