UFUNDI NA MBINU KUIMALIZA RWANDA KESHO ~ KOCHA MAYANGA
Kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Salum Mayanga amesema ana imani kubwa sana kwamba timu yake itafanya vyema katika mchezo wa kesho dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda katika mchezo wa kufuzu wa CHAN.
"Tumefanya mazoezi mazuri sana toka tufika mkoani hapa na tuna imani ya timu yetu kufanya vyema"
Mayanga alisema.
Kocha huyo wa zamani wa timu ya Tanzania Prisons na Mtibwa Sugar alisema hategemei mchezo wa kesho kuwa rahisi.
"Mechi za mashindano hakuna mechi ambayo ni nyepesi tunategemea mchezo utakuwa mgumu. Rwanda ni timu iliyobora katika ukanda wetu ambayo tunaifahamu vizuri na wao wanatufahamu vyema.
Matumaini yangu tutacheza kwa kujituma na kwa ufundi na mbinu zilizo nzuri na tutapata mafanikio kwa kushinda mchezo wetu" Mayanga alisema.

No comments