*SINGIDA UNITED USIPIME: YATAMBULISHA BUS LAO WAKIELEKEA MWANZA KUANZA KAMBI*

Timu ya soka ya Singida United imetangaza kuanza rasmi kambi ya kujiandaa na michuano ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo inataraji kuanza kutimua vumbi katikati ya mwezi Agosti.

Timu hiyo iliyopanda daraja inataraji kuanza kambi kesho jijini Mwanza chini ya kocha mkuu Hans Van Pluijm wakiwa na wachezaji 23 wakiwemo 6 wa kimataifa, wanne wapya kutoka hapa hapa Tanzania na 11 waliopandishwa kutoka timu za vijana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa habari wa Singida United Festos Sanga Amesema pamoja na mambo mengine amesema ukarabati mkubwa wa uwanja wao wa nyumbani wa Namfua unaendelea vizuri, tayari nyasi mpya zimepandwa na ujenzi wa vyumba vya kubadilishia nguo na vyoo tayari umekamilika kwa msaada mkubwa wa wabunge wa CCM katika mkoa wa Singida.

Aidha, timu hiyo imetumia nafasi hiyo kutambulisha basi lao jipya aina ya Dragon ambalo ndilo litakalotumika katika safari zao za barabarani.

Sanga amewataka mashabiki wa soka wanaoihusisha Singida na vilabu vya Simba au Yanga kuachana na dhana hiyo kwa sababu Singida UTD ni klabu inayojisimamia yenyewe katika kila kitu.


No comments

Powered by Blogger.