NDEMLA,MAHUNDI NA KABWILI WAONGEZWA TAIFA STARS


Image result for ndemla


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Salum Mayanga amekipa nguvu kikosi chake ambacho kiliibuka na ushindi wa tatu kwenye michuano ya COSAFA baada ya kuwaita kikosini wachezaji 6 toka timu mbalimbali.

Said Hamis Ndemla kiungo mshambuliaji wa Mabingwa wa kombe la FA Simba ni mmoja kati ya nyota walioitwa na Mayanga ambaye ana jukumu pevu mbele yake kuhakikisha Stars inafuzu Kombe la mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani.

Sambamba na Ndemla kiungo wa Azam FC Joseph Mahundi, Kelvin Kiduku toka MajiMaji ya Songea,Boniface Maganga wa Mbao FC ya Mwanza na Chipukizi wawili Athanas Mdam toka Alliance Academy na kipa wa Serengeti Boys Ramadhani Kabwili.

Taifa Stars Jumamosi hii itakua na kibarua kigumu kucheza dhidi ya Rwanda kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kwa kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani ambapo fainali zake zitafanyika Nchini Kenya mwakani.

No comments

Powered by Blogger.