LWANDAMINA AREJEA TAYARI KWA MAWINDO YA MSIMU MPYA.
Kocha wa Yanga George Landamina amewasili nchini
jana kutokea Zambia alikokua kwa mapumziko baada ya msimu uliopita ambapo
aliwaongoza Yanga kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Kuwasili kwa kocha huyo kumeondoa minong'ono
iliyokuwepo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini kwamba kocha huyo hatorejea
kuwanoa mabingwa hao kwa msimu mwingine.
Baada ya kurejea, Lwandamina amesema atakaa na
viongozi wa Yanga kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kuhusu maandalizi ya
timu hiyo kama yalivyopendekezwa katika ripoti yake ambayo tayari
alishaiwasilisha kwao.
Yanga wamekua wakiendelea na usajili wa wachezaji
sambamba na kuwasainisha mikataba mipya wale ambao mikataba imemalizika ambao
kwa mujibu wa viongozi wa klabu hiyo ni kwamba wanasajili kwa mapendekezo ya
kocha wao

No comments