KUIONA EVERTON DAR ES SALAAM BUKU 3 TU.

Wakongwe wa Ligi kuu ya England klabu ya Everton wataweka historia nchini Tanzania watakapocheza kwa mara ya kwanza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Wakongwe wa soka la Kenya klabu ya Gor Mahia.

Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja mkuu wa Taifa Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya England kwa klabu ya Everton lakini fursa pia iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa klabu hiyo kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya SportPesa ambao wameingia nchini mwaka huu na kuweka fedha nyingi kwenye udhamini wao kwa vilabu mbalimbali vikiwemo Simba na Yanga.

Viingilio katika mchezo huo vitakua shilingi elfu 3 kwa kiingilio cha Chini na elfu 8 kiingilio cha Juu na mchezo utachezwa majira ya jioni.

Tayari uwanja wa Taifa uko kwenye hatua za mwisho za marekebisho kwaajili ya mchezo huo.

No comments

Powered by Blogger.