AJIBU ASAINI RASMI YANGA MIAKA MIWILI.

Mshambuliaji mwenye kipaji maridhawa hapa nchini, Ibrahim Ajibu Migomba, amejiunga rasmi na mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara Yanga ya Dar es Salaam.

Ajibu ambaye hivi karibuni ilitangazwa kwamba wameshindwana na klabu yake ya Simba kuhusu mazungumzo ya kusaini mkataba mpya, amesaini kandarasi ya miaka miwili Jangwani mbele ya viongozi mbalimbali wa kamati ya usajili ya klabu hiyo.

Huu ni usajili mpya wa pili rasmi kutangazwa na Yanga tangu msimu huu wa usajili uanze baada ya kumsajili beki Abdalah Haji kutoka Taifa Jang'ombe ya visiwani Zanzibar.

 Pamoja na Ajibu, wachezaji wengine wa ndani wanaotajwa kuwa kwenye rada za Yanga ni pamoja na Raphael Daud wa Mbeya City, Gardiel Michael na Himid Mao wa Azam FC pamoja Pius Baswita ambaye inasemekana tayari amekwishamalizana na viongozi wa Yanga.

No comments

Powered by Blogger.